Je, ni wakati gani mwanamke mjamzito anatakiwa kuacha kufanya mapenzi?
Ijapokuwa wapo wanawake wengi ambao wanaweza kabisa kuendelea kufurahia kufanywa hadi siku wanakwenda kujifungua , kuna baadhi ya nyakati mshauri wako wa afya anaweza kukushauri kuacha ngono kutokana na moja au yote kati ya yafuatayo:- umekuwa na tatizo la kujifungua kabla ya muda muafaka kabla ya ujauzito ulio nao
- umetokewa na tatizo la kutokwa na damu kwenye uke
- umekuwa ukitokwa na ute fulani ambao wataalamu wanauita kwa jina la "amniotic fluid"
- umekuwa na tatizo la kwenye mlango wa uzazi, ambalo kitaalamu linajulikana kama cervical incompetence
- kondo la nyuma limesambaa na kuziba kabisa mlango wa uzazi na kuanza kujitokeza kwa nje (placenta previa)