Wednesday, December 4, 2019

Dunia haijali mazuri yako ila ubaya wako, jiamini songa mbele

Siku moja mwalimu wa shule aliandika ubaoni kama ifuatavyo:

9×1=7
9×2=18
9×3=27
9×4=36
9×5=45
9×6=54
9×7=63
9×8=72
9×9=81
9×10=90

Alipo maliza kuandika tu, akaona wanafunzi wote walikua wanamcheka, kwasababu alikua amekosea swali la kwanza. Mwalimu aliwatazama wanafunzi, kisha akawaambia yafuatayo:

`"Nimejikosesha lile swali la kwanza makusudi, kwasababu nilihitaji mjifunze kitu kimoja muhimu sana. Mnapaswa kujua namna ambavyo dunia inaweza kuwachukulia. Unaona hapo, nimeandika kwa usahihi mswali tisa (9), lakini hakuna kati yenu aliyenipongeza kwa hilo; wote mmecheka na kunilaumu kwasababu ya kosa moja tu nililofanya."`

Hivyo, hili ni somo kwenu:

`"Dunia haijali mazuri unayofanya hata ukiyafanya mara milioni, lakini fanya baya moja uone jinsi watakavyo kulaumu...Hata hivyo usikatetamaa, MARA ZOTE SIMAMA IMARA NA USHINDE VIKWAZO VYOTE, JIAMINI." `