Wednesday, January 23, 2019

Sms nzuri za mahaba unazoweza kuzitua usiku huu

Sms nzuri za mahaba unazoweza kuzitua usiku huu 
Samahani kutabasamu kila wakati unapokuwa karibu nami, samahani macho yangu yanaangaza unapokuwa hapa, samahani nakupenda sana na siwezi kujizuia kuficha penzi langu kwako....
*********

Nimefumba macho na kukuwaza wewe. Wakati mwingine nikiwa peke yangu akili yangu inahangaika juu yako, kila ninapokukosa machoni moyoni nateseka, ninapokukosa kitandani chakula hakipiti vema kooni, mawazo ya penzi lako yananifanya nikae nikitabasamu.
*********

Manukato yako ninapokukumbatia hubaki mwilini mwangu, unaponibusu nahisi maraha ya mahaba, utamu wa penzi ni kuridhishana, naomba leo unipe raha za mwili wako nami nikupe za mwili wangu, ahsante sweet wangu kuwepo karibu yangu....
**********

Bila shaka umeianza siku yako kwa uso wenye tabasamu, na furaha ya moyo wako, umeamkaje mpenzi wangu nakutakia siku njema. Siku ya leo ni muhimu kwangu kuwa na wewe, jioni tuonane mpenzi...
*********

Umeamkanje mpenzi bila shaka umzima. Nakutakia siku njema yenye furaha na upendo.Fanya kazi kwa bidii tujenge familia yetu iwe bora, kazi muhimu lakini wakati mwingine kumbuka penzi leu....
***********

Hello sweet, amka, pokea zawadi ya asubuhi uliyojaa upendo, yenye uangalifu na kufungwa na maombi ili kukuweka salama na kuwa na furaha siku nzima! Kuwa mwangalifu mpenzi wangu.
*********

Angalia nje ya dirisha, jua limewaka kwa ajili yako, maua yamechanua kwa ajili yako,
Ndege wanaimba kwa ajili yako .Unajua nini  kwasababu usiku niliwaomba wakutakie asubuhi njema.
**********

Nashukuru mpenzi wangu kwa kuniamsha, nimewahi kazini kuniamsha kwako kwa bashasha na furaha, bada ya kuota ndoto nzuri... nikiwa na wewe kunanifanya nijisikie furaha siku nzima. Nami nakutakia asubuhi njema.
*******

Dear mikono yako inaponigusa nahisi raha nisizoweza kuziandika, unaponisogezea midomo na kuikutanisha, nasisimka..unaponishika kiuno mwili unapatwa na joto la raha, unaponitamkia unanipenda moyo wangu hufarijika.Penzi lako haliishi utamu, ukweli nakuambia..leo hadi milele.
**********