Aliwahi kuulizwa, JE KUNA TOFAUTI GANI KATI YA KUPENDA NA KUTAMANI?
Buddha alijibu; "Ukiliona Ua zuri ukalitamani, utalichuma. Lakini ukilipenda utalimwagia maji, kuliwekea rutuba na kulijali ili lizidi kuchanua vyema".
Jibu hilo ni fumbo tosha kabisa kuonyesha utofauti uliopo kati ya kupenda na kutamani.
Vijana wengi wa sasa wanashindwa kutofautisha tofauti kati ya Kupenda na Kutamani na ndio maana Mahusiano ya Wakati wa sasa, mengi sio ya kudumu kwa wakati mrefu.