Wednesday, January 16, 2019

Je, kufanya wakati wa ujauzito kunaharibu au kumdhuru mtoto?

Je, kufanya wakati wa ujauzito kunaharibu au kumdhuru mtoto?
Kiumbe kilicho tumboni wakati wa ujauzito huwa kinakingwa na ute maalum unaojulikana kitaalamu kwa jina la "amniotic fluid" ndani ya mji wa uzazi, pamoja na kuta za mji wenyewe wa uzazi.

Hakuna namna ambavyo muhogo unaweza kupita na kufika mahali mtoto anapokuwa anakua huko ndani, au zile mbegu kuwa zitapita moja kwa moja na kwenda kumdhuru mtoto.

Kumekuwa na ule msemo wa kuwa kufanya wakati wa ujauzito ni kulea mimba, watu wakiamini kuwa mbegu huwa zinakwenda moja kwa moja kwenye kiumbe.

Dhana hii ni potofu. Kama kilivyo chakula cha kawaida mtu anapokula, ndivyo ambavyo mbegu nazo huwa hivyo.

Kila kitu kwanza lazima kiingie katika mfumo wa kawaida wa usafirishaji wa virutubisho vilivyo sahihi kuelekea kwenye kiumbe husika.

Hii ikimaanisha kuwa mbegu nazo huingia katika mfumo huo huo, huchujwa na kile kinachoonekana kuwa ni kirutubisho kitasafirishwa kwenda kulea kiumbe, ilhali yale makapi lazima yatatoka.

Tofauti pekee hapa ni kuwa, "mbegu za kiume zina protini nyingi", hii ikimaanisha kuwa sehemu kubwa ya kile kinachomwagwa kwenye uke wa mjamzito, kina nafasi ya kutumika kwa ajili ya kuongeza rutuba kwa kiumbe kinachokuaa ndani ya tumbo.

Na nyingine zinaweza kutoka tu zenyewe bila matatizo yo yote.