Wednesday, January 16, 2019

Je, kufanya wakati wa ujauzito kunaweza kusababisha ujauzito kuharibika?

Je, kufanya wakati wa ujauzito kunaweza kusababisha ujauzito kuharibika?
Hili pia ni miongoni mwa maswali na hali ambazo zimekuwa zikiwachanganya watu wengi, waume kwa wanawake.

Ila ukweli ni kwamba, kufanya hakuhusiani na kuharibika kwa mimba au kujifungua kabla ya wakati muafaka.

Kwa kawaida, kuharibika kwa mimba hutokana na sababu zingine tofauti kabisa, ikiwa ni pamoja na kizazi cha mwanamke kuwa na matatizo hasa katika kuhimili ukuaji wa kiumbe tumboni na sababu zingine za kimazingira.

Wala sio kwa sababu ya kitu ambacho unakifanya au hukifanyi.