Wednesday, January 16, 2019

Je, ni sahihi kufanya mapenzi ikiwa mwanamke wako ni mjamzito?

Je, ni sahihi kufanya mapenzi ikiwa mwanamke wako ni mjamzito?
Ndio, hakuna tatizo lolote kwa mwanamke kuendelea kufurahia mapenzi na mumewe au mpenzi wake wakati anapokuwa mjamzito.

Wataalamu wanaeleza kuwa, ikiwa ujauzito ulioubeba haukupi shida yoyote ile na unajisikia uko poa, basi hakuna hatari yoyote ile ikiwa utataka kufanya.

Tatizo pekee ambalo huwa linawakumba wengi wa wanawake wakiwa wajawazito ni kuwa, huwa wanapoteza hamu ya tendo lenyewe wanapokuwa katika hali hii, au kushindwa kumudu kutokana na kujisikia uchovu muda mwingi.

Ingawa pia wapo wanawake ambao wakiwa katika hali hii ndio kwanza, wanakuwa wanajisikia kukereketwa huko kwenye ki**i kupita maelezo, na wanatamani muda wote wafanye mapenzi.
Wapo baadhi ya wanawake ambao wanakuwa wako normal kimwili, lakini kisaikolojia wanakuwa na ile hofu ya kuwa kufanya kunaweza kuwaharibia mimba zao, fikra ambazo huwatoa kabisa katika mstari wa kufurahia tendo hili.

Kwa hiyo, ikiwa mwili wako uko poa, na madaktari wamekwambia kiumbe kinakua bila shaka, na unaweza kwenda kazini, huna haja ya kujibania utamu wa mumeo au kumbania mumeo.