Tuesday, January 15, 2019

Tabia 16 za watu wasio na mafanikio na wasio na mazingira ya kufanikiwa

Tabia 16 za watu wasio na mafanikio na wasio na mazingira ya kufanikiwa
1. Ni watu wenye tabia ya kujipendelea wao wenyewe, watu wenye umimi na ubinafsi wakati wote

2. Ni watu wenye tabia ya ubishi na kupinga kila jambo, hususani lile ambalo mwingine amelisema ama kulizungumza, kwao hoja ya mwingine sio hoja bali hoja yao ndiyo hoja pekee.

3. Ni watu wenye visasi na mafundo ya moyoni hata katika vitu vidogo na visivyo vya msingi, wanaweza kuzira kirahisi tena kwa muda mrefu bila hata sababu ya msingi

4. Wanaumizwa sana pale mwingine anapopewa pongezi au kusifiwa au kupewa ushindi, kiu yao ni kwamba pongezi zote na sifa zote na ushindi wote uwe wakwao. Mara mwingine anapoonekana kushinda basi wao hujifanya ndio waliokuwa chachu au wasababishaji wa ushindi huo na kwahivyo wanataka wapongezwe wao au mchango wao kukubalika mbele za watu

5. Ni watu walalamishi sana na wenye kulaumu kila mazingira, huwalaumu wengine pale wao wanapoonekana kushindwa, wakishindwa au kufeli wao basi huzitupia lawama kwa watu wanaowazunguka, utasikia wakisema “kama asingekuwa fulani basi nisingeshindwa hivi, yeye ndiyo amesababisha mimi kufeli au kutofanya vizuri”

6. Wanapenda na wala hawaoni tatizo kupoteza muda, anaweza kukaa mbele ya televisheni masaa na masaaa bila kujali muda unavyopotea

7. Mara nyingine hujaribu kujiwekea mpangilio wa siku wa nini atafanya na wakati gani lakini kamwe hawawezi kufwata walichokipanga wenyewe

8. Ni waoga na wapinzani wa mabadiliko hata kama hawanauhakika nini asili ya mabadiliko hayo

9. Mara zote hudhani na hufikiri kuwa wanajua kila kitu, ni ngumu sana kuishi na mtu wa aina hii kwa maana wakati wote ni ngumu kumbadili au kubadili lile analoliwaza au kulifikiri maana yeye anauhakika kuwa anafahamu kuliko mwingine yeyote

10. Katika kila wanalofanya wao husukumwa na mawazo au kiu ya kujua nini anafaidika nacho, kama yeye hapati manufaa ya moja kwa moja katika chochote afanyacho basi hawezi kushiriki chochote. Watu wahivi ni ngumu sana kusaidia mtu mwingine au kutoa mchango wa hali na mali kwa jamii maana wao huona kuwa hauna faida za moja kwa moja kwake.

11. Ni watu wanaopenda kuwazungumzia wengine, huzungumzia madhaifu ya watu na kushindwa kwa wengine, hata siku moja hawawezi kujadili mafanikio ya mtu mwingine

12. Mara nyingi ndani ya mioyo yao huwaza au kutamani wengine washindwe au wasiendelee, tena sio kutamani tu bali huumia wanapoona wengine wanafanikiwa

13. Sio wepesi wa kutoa taarifa muhimu kwa wengine, ni wafichaji wa taarifa za muhimu maana ndani yao wanakiu ya kuzuia maendeleo yaw engine au kuona wengine wanafanikiwa

14. Hawafahamu wala hawajui nini wanatamani wala ni nini wanataka maishani, kwa maana hiyo ni ngumu kufikia katika mustakabali wowote

15. Ni watu wenye hasira au kushindwa kujizuia kuonyesha hasira zao

16. Ni watu wasio na malengo, wasioweka malengo binafsi na wala hawawezi kuyafuata malengo yao, kwa hali hiyo basi inakuwa ngumu kufikia mafanikio maishani mwao.