Sunday, December 1, 2019

Je, ni muda gani sahihi wa wapenzi kukutana kimwili?

Je, ni muda gani sahihi wa wapenzi kukutana kimwili?
Ingawa hatutoshangazwa majibu ya wengi watakaosema kuwa hawajui muda sahihi wa kukutana faragha na wapenzi wao.

Tunajua kuwa watu wengi hupendelea kukutana na wapenzi wao nyakazi za giza hasa (kabla ya kulala), lakini kutokana na tafiti zilizofanywa na wanasayansi hivi karibuni, zinaonyesha kuwa kiwango cha homoni za Testosterone (vichochezi) huzalishwa kwa kiwango kikubwa sana nyakati za asubuhi.

Mtaalamu wa maswala ya mahusiano Geraldine Myers katika jarida la Daily Mail Report, alisema “nyakati za asubuhi ni muda sahihi wa wapenzi kukutana kimwili kwasababu kiwango cha nguvu kati ya wanaume na wanawake huwa katika kilele cha juu sana nyakati hizo tofauti na nyakati zingine; lakini pia fikra zao zinakuwa hazijatawanyika”.

Hawakuishia hapo. Wakati asubuhi imeonekana kuwa muda sahihi wa wapenzi kukutana kimwili, watafiti wame kugundua pia kuwa“SAA 05:48AM (Saa kumi na moja na dakika arobaini na nane alfajiri) ni muda sahihi kabisa kwa wapenzi kufurahia mahaba yao kwakuwa ni muda ambao wapenzi huwa katika kilele cha nguvu zao”.

Kutambua muda sahihi wa wewe na mwenzi wako kufanya mapenzi, ni njia pekee ya kuiamsha hamasa ya mpenzi wako kutaka kufanya mapenzi na wewe mara kwa mara