Ni baada ya muda gani toka kujifungua mwanamke anaweza kuendelea kufanya mapenzi?
Iwe kwa njia ya upasuaji au kwa njia ya kawaida, inaeleweka wazi kuwa baada ya kujifungua, mwanamke anakuwa na hali fulani ya mwili kuchoka, hali ambayo ni ya kawaida.Ingawa wapo ambao wanaweza kujihisi wanamudu kushiriki tendo la ndoa kabla, lakini wataalamu wanashauri kuwa wakati mzuri wa kurejea kufanyana na mwenzio baada ya kujifungua, inakuwa ni baada ya kupita wiki sita.