Wednesday, January 23, 2019

Sms mpya na kali za mapenzi 2019

Sms mpya na kali za mapenzi 2019
Siku zote kwangu ni sherehe ni wewe unishereheshaye,  ukweli usio na kejeli mapenzi yako yanatii kiu yangu, moyoni mwangu nimeridhia... Nakupenda daima mpenzi!
****

Ahsante Mungu shukrani kwako mama, pongezi kwako mpenzi kuwa wangu mtetezi kwenye jahazi la mapenzi, ufundi na ujuzi unao hasa tuwapo wawili chumbani. Penzi lako halichakai daima huzaliwa jipya.
******

Mapenzi ni upepo, mimi sivumi na kupotea, mapenzi ni mahaba sili nikamaliza, nikimaliza nitakula nini kesho? Nakuahidi kukupenda leo hata kesho ukiwepo na hata usipokuwepo.
*****

Imara hautikisiki, kakamavu halishikiki penzi langu kwako ni nuru daima halizimiki.
*****

Mapenzi si usanii ukiigiza utashindwa, mapenzi yanatoka moyoni wengi walioigiza walishatengana, mpenzi wangu usiniache.
******

Mimi si mtume hakuna mwadamu aliyestahili usiniache nitajirekebisha na nitaongeza bidii.Naahidi kuwa mpenzi mpya na bora kwako na si bora mpenzi.
*******

Mpenzi usiende mbali nami, njoo ufaidi utamu usioisha hamu, nitakupa mwili wangu ucheze nao hadi asubuhi, nitakulisha unachokitaka, sitakubania kwani naogopa wengine wanaweza kukupa... njoo leo uniambie unataka nini?
*******

Wengine waliachana wakati bado wanakupenda, wengine waliachana sikuchache baada ya kuchokana, wengine waliachana walipopata pesa, wengine waliachana walipopata wapenzi wapya..naomba nikutoe wasiwasi kuwa siwezi kukucha hata nipewe mamlaka ya kuogoza dunia nzima.
******

Nipe niridhike, nionjeshe usinilambishe nikigonga unikaribishe na ndoa yetu tuiharakishe.
******

Mapenzi mazuri yanasifa zifuatazo, kuridhishana, kupeana bila kubaniana, kubusiana, kusaheshimiana, kujaliana, kusubiriana, kusikilizana.Je, utaweza kujifanyia yote hayo? Nijibu mpenzi...
******

Utakuwa wangu wa maisha daima na penzi letu litakuwa kama mfuko wa hazina, tutalitunza kama zaidi ya mboni ya jicho.
******