Mambo 7 ambayo utayapata ukila Mayai
Mayai yana wingi wa protini,ni vizuri kutumia mayai kwa kujenga mwili wako. Haya ndio mambo yatakayo tokea katika mwili wako ukila mayai;1. Inapunguza matatizo ya moyo
Japo mayai yanaweza kuongeza choresterol kwa baadhi ya watu ila utafiti unaonyesha ulaji wa mayai una uwezo mkubwa wa kufyeka hatari ya kupata matatizo ya mishipa ya moyo
2. Inaongeza Kinga ya mwili
Ukitaka uwe mbali na maambuki ya bacteria au virusi,tumia yai kwa kila mlo. Yai moja lina asilimia
22 ya RDA ya Selenium, virutubisho vinavyosaidia na kuongeza kinga ya mwili
3. Inarekebisha choresterol
Mayai yanaweza kurekebisha mfumo wa choresterol. Mayai yana uwezo wa kuongeza HDL iliyo nzuri na inaongeza ukubwa wa chembe za LDL
4. Itakuongezea vitamins
Mayai yana asilimia 15 za RDA ya vitamini B2,pia inajulikana kama riboflavin. Itakusaidia kubadilisha chakula na kuwa mafuta ambayo itakusaidia kutengeneza nguvu.
5. Kurutubisha ngozi na nywele
B-complex vitamins vitaipa afya ngozi yako, nywele, macho na ini (zaidi ya B2,yai pia lina B5 na B12 Vitamin)
6. Inakinga Ubongo wako
Mayai ni chakula cha ubongo,hii ni kutokana na wingi wa virutubisho aina ya choline.
7. Ina imarisha Mifupa na Meno
Mayai yana vitamini D, ambayo ni muhimu kwa afya ya mifupa na meno.