Kwa nini mara nyingi mvulana ni mwepesi sana katika kuanzisha kufanya mapenzi?
Kwa kawaida inakubalika kuwa wavulana ndiyo waaanze kuonyesha ishara za kujamiaana na tafiti zimeonyesha kwamba mara nyingi mwanaume anafikia mshindo kabla ya mwanamke. Hii ni ukweli katika sehemu nyingi za dunia.Baadhi ya wavulana wanatumia vibaya uwezo wao wa kufanya mapenzi. Wanafuatafuata wasichana na kuwatongoza ili wafanye mapenzi katika umri mdogo. Hata hivyo kujamiiana katika umri mdogo kunaweza kusababisha athari nyingi kama vile mimba isiyotarajiwa au kuambukizwa magonjwa ya zinaa.
Kwa hiyo, wavulana wanashauriwa kuwa wavumilivu licha ya mivuto hiyo ya kutaka kujamiiana, kwa sababu kwa njia ya kujamii anaovyo mnahatarisha maisha yenu ya baadaye.
Kuna njia nyingine za kuonyesha mapenzi, kama vile kubusu, kukumbatia, kushikana mikono na hata kupiga punyeto.
Kimaumbile, mara nyingi mwanaume anafikia mshindo haraka zaidi kuliko mwanamke. Lakini, mkihakikisha kwamba mwanamke ni tayari kwa kujamii ana na kama mmechukua muda wa kutosha kujiaanda vizuri, mnaweza kufikia mshindo pamoja. Hivyo kuwaletea raha na starehe wote wawili.