Faida 6 za tendo la ndoa wakati wa ujauzito
Wataalamu wa mambo ya afya wanasema kuwa kukutana kimwili wakati wa ujauzito hakuwezi kuzuia mwanamke na mwanaume kutimiza haja zao ikiwa hakutakuwa na hatari yeyote kiafya kwa mama na mtoto.
Kwa kawaida wataalamu wanashauri kuwa angalau wiki mbili hadi tatu kabla ya mama kujifungua kuacha kushiriki tendo hilo kwani kisayansi shahawa za mwanaume huwa na kemikali zinazoweza kuanzisha uchungu wa mwanamke kuzaa kabla ya wakati sahihi wa kujifungua.
Muhimu kuzingatia ni kuhakikisha kuwa ni lazima itafutwe njia salama ya kukidhi haja bila kuathiri afya ya mama na mtoto.
Zaidi wataalamu wa afya wanasema kuwa kukutana kimwili wakati wa ujauzito huwa na faida nyingi ambazo ni.
1. Huongeza msisimko wa misuli ya nyonga hivyo kumuandaa vizuri mama wakati wa kujifungua na kumsaidia pia kuponya majeraha mapema baada ya kujifungua.
2. Hupunguza kwenda haja ndogo mara kwa mara.
3. Huendelea kuimarisha mapenzi na mahusiano.
4. Ni sehemu ya mazoezi hivyo humuandaa mama vizuri kwa ajili ya kujifungua.
5. Hupunguza msukumo wa damu mwilini, kwani ki kawaida mwili hutengeneza zaidi ya 50% ya vimiminika vipya wakati wa ujauzito ambavyo ni maji na damu hivyo msukumo wa damu huongezeka.
Lakini kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za afya protini zinaopatikana kwenye shahawa ya mwanaume. huimarisha ulinzi wa mwili wa mwanamke mjamzito, hivyo mwanamke mjamzito anayeshiriki tendo hili huwa na faida ya kutokuugua magonjwa madogo madogo mara kwa mara kuliko yule asiyefanya kabisa.
Aidha ni muhimu kufahamu kuwa endapo daktari atashauri wawili hao kutoshiriki tendo hilo kutokana na sababu za kitabibu na kiafya ni vyema wawili hao kufuata ushauri wa daktari kwenda kinyume na ushauri wa daktari kunaweza kuleta madhara makubwa hasa kwa mama na mtoto.