Thursday, January 24, 2019

Vijue vyakula vya asili vinavyokuza makalio - Ladies

Vijue vyakula vya asili vinavyokuza makalio
IMEKUWA ni kawaida kwa akina dada wa siku hizi kupenda kuwa na makalio makubwa kwa kile wanachoamini huchangia kuvutia wanaume.

Huenda kuna ukweli juu ya madai hayo ingawa bado hakuna utafiti uliothibitisha hoja hiyo. Kutokana na dhana hiyo iliyojengeka vichwani mwa dada zetu hao, wamekuwa wakifanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanakuwa na makalio makubwa wakiamini watakuwa wamewafunga na kuwadhibiti kabisa wanaume wao au kuwavutia wengine zaidi.

Wamekuwa wakidiriki hata kufanyiwa upasuaji au kutumia dawa za kisasa na hatimaye hujikuta wakitumia fedha nyingi kupambana na madhara yatokanayo na njia hizo. Wakati hayo yakiendelea, kuna habari njema kuwapo kwa njia mbadala ya wanawake wenye nia ya kukuza makalio yao ya kutumia vyakula vya asili.

Vyakula vyenye Protini, Protini ina umuhimu mkubwa mwilini achilia mbali kwa mwanamke anayetaka kuongeza ukubwa wa makalio yake. Baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha wenzao kuwa vyakula vya protini ni kwa ajili ya watu wanaobeba vyuma. Si kweli. Kila binadamu anahitaji kiasi cha protini ili kuimarisha afya yake.

Mwanamke anayependa kuwa na makalio makubwa atahitaji kuongeza matumizi ya vyakula vya protini. Mfano wa vyakula hivyo ni mayai, maharage, mboga za matunda na viazi vitamu. Ikiwa atapata japo gramu 15 hadi 30 ya protini kwa kila mlo. Vyakula vyenye mafuta Pia wanawake wenye nia ya kuongeza ukubwa wa makalio yao wanahitaji vyakula vinavyozalisha mafuta. Mfano; samaki, nazi, korosho na karanga.

Mboga za majani Mboga za majani zina virutubisho mbalimbali vinavyosaidia kukuza makalio. Kwa yeyote anayetaka kuongeza makalio yake, anatakiwa kula kwa wingi kadiri awezavyo vyakula vinavyohusisha mboga za majani bila woga.

Mboga hizo zinaweza kuambatana na ulaji wa spinachi, nyanya na mazao mengine ya majani kama hayo. Mchanganyiko wa vyakula hivyo kwenye mpangilio wa mlo, huweza kumfanya mwanamke kutimiza kusudio lake la kuwa na makalio makubwa bila kutumia njia za kisasa ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa na madhara.