Makosa 7 ya kijinga ambayo wanaume hufanya katika mahusiano
Ni vizuri kufundishana. Kuna mambo ambayo mtu anaweza kufanya pasi na kujua kuwa anafanya makosa. Ikija katika masuala ya mahusiano, wanaume wengine huchukulia kama mzaha. Wakishafaulu kutongoza na kumteka hisia mwanamke, wao hujisahau na kuanza kuishi nao kama mtu wa kawaida.Leo tumekuja na ujuzi wa kukuonyesha makosa ambayo unaweza kuwa unayafanya bila kujua kuwa yana athari. Kiufupi ni makosa ya kijinga ambayo yanaweza kuepukika kirahisi iwapo utayafuatilia.
Hii ni muhimu kwa kuwa ukiachana na makosa haya basi unaweza kudumu katika mahusiano marefu na mpenzi wako zaidi. Zama nasi.
1. Kuwa dume-toto
Hii ni tabia ya kuwa umeingia katika mahusiano na mwanamke lakini bado una tabia za kitoto. Hapa unakuwa na tabia ambazo hazina misimamo, unakuwa na hisia haraka na hujiamini.
Kwa mfano uko na huyu mwanamke lakini kama kuna kitu kimefanyika wewe ndio wa kwanza kukimbia ama kulia. Wewe huna misimamo katika maisha, mara leo unasema hivi na kesho unabadilisha. Na pia hujiamini. Mwanamke anataka mtu ambaye anaweza kumsimamia.
2. Unasahau kujijenga kibinafsi
Kosa lengine ambalo wanaume hujipata katika uhusiano ni pale ambapo wanatelekeza majukumu yao ya kujiendeleza kimaisha. Wanasahau mambo ambayo walikuwa wakifanya ama walikuwa wakitarajia kufanya kabla kuingia katika uhusiano wa kimapenzi.
3. Kusahau marafiki zako
Ni kawaida kupunguza mawasiliano na marafiki zako pindi ambapo utaingia katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamke. Lakini hii haimaanishi kuwa hufai kuwasiliana nao kabisa. Marafiki zako watabaki kuwa marafiki zako. Mwanzo kabla kuingia katika mahusiano marafiki zako walikuwepo. So swala hili usilipuuze kwa kuwa bado marafiki zako wako na umuhimu mkubwa katika maisha yako.
4. Kuacha kufukuzia ndoto zako
Kama tulivyoeleza katika hoja ya pili, maisha hayaishi pindi utakapoingia katika mahusiano. Mahusiano kikawaida yako na yatazidi kuwapo. Usikatishe furaha ama ndoto zako. Kama ulikuwa una mipango ya kufanya jambo fulani katika maisha basi ni jukumu lako kuhakikisha kuwa ndoto hio inatimia.
5. Kuchizika naye
Kuna wanaume wengine wakiingia katika uhusiano na mwanamke basi wanajisahau kabisa. Maisha yao yote yanabadilika na kuzungukwa na mwanamke huyu. Wako tayari kufanya lolote au chochote kwa sababu ya huyu mwanamke. Well, hii si tabia nzuri kwa sababu huyu mwanamke hataenda mahali. Atakuwa na wewe muda mrefu hivyo hupaswi kufanyika kana kwamba huyo mwanamke ni kila kitu kwako.
6. Unakuwa na wivu
Hili ni kosa kubwa ambalo baadhi ya wanaume hujikuta wanafanya. Kuwa na wivu ni ishara ya kuonyesha kuwa hujiamini. Awali tumeongea kuhusu umuhimu wa kuwa na tabia za mwanaume kamili.
7. Kuishi katika mzunguko
Hii itatokea pale ambapo wewe na mpenzi wako mnaishi katika maisha ya kujirudia. Ni kama mumetengeneza ratiba ya kuyapeleka maisha yenu. Jumamosi hadi Ijumaa kuna ratiba ambayo munaifuata. Kuishi katika maisha kama haya kunaboesha na kuchosha. Mahusiano yenu hayana utofauti na vile mwaka jana ilivyokuwa. Mwanaume anapaswa kubadilisha mtindo huu. Mfano anapaswa kumsaprize mwanamke na mambo tofauti tofauti ambayo hakuyatarajia.
Hizi ndizo baadhi ya makosa ambayo wanaume wengine hujipata wakiwa katika mahusiano. Iwapo uko katika mahusiano na mwanamke, basi jaribu kadri uwezavyo kuhakikisha kuwa unaacha tabia yeyote ambayo tumeweza kutaja.