Tuesday, January 29, 2019

Fahamu faida za pweza kwenye afya ya mwanadamu.

Fahamu faida za pweza kwenye afya ya mwanadamu.
Samaki aina ya Pweza amejawa na wingi wa virutubisho ambavyo husaidia mwili kujikinga dhidi ya magonjwa kama vile saratani kama saratani ya mdomo, utumbo mkubwa, tumbo, matiti, shingo ya kizazi na pia kansa ya mapafu.

Pweza amejawa na virutubisho vinavyosaidia kuongeza ashki (hamu) na kuboresha tendo la ndoa. Hii ni kutokana na uwepo wa virutubisho aina ya protini na madini ya selenium.

Aidha Pweza humsaidia mwanamke kuwa na sifa halisi za kike na pia mwanaume kuwa mwanaume wa shoka. Kwa mwanaume humsaidia kuwa na misuli iliyojengeka vizuri na hivyo kuweza kumtofautisha mwanaume na mwanamke.

Faida ya nne ni kuwa pweza ina virutubisho vinavyosaidia kuukinga mwili dhidi ya kupungukiwa na uwezo wa ubongo hasa kwa wenye umri mkubwa. Kitaalamu tatizo hili huitwa Alzheimer. Pweza huwasaidia walaji kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Pumu .

Wataalamu wamegundua kuwa mlaji wa pweza yupo katika hatari ndogo ya kuugua ugonjwa wa pumu. Hata wenye ugonjwa huo huweza kupata virutubisho vya kupunguza athari za ugonjwa.Pweza husaidia mwili kufanya kazi zake vizuri ikiwamo mmeng’enyo wa chakula, upumuaji na hata mzunguko wa damu.

Minofu ya pweza huusaidia mwili kuzalisha Haemoglobin ambazo ni muhimu katika damu. Hii ni kwa sababu pweza ana madini aina ya shaba ambayo ni muhimu kwa kazi hiyo. Kwa upande wa kina mama, pweza husaidia katika uzalishaji wa maziwa pindi wanapojifungua .

Faida nyingine waipatayo watumiaji wa supu na minofu ya pweza ni kuwa huongeza madini joto mwilini. Virutubisho vilivyomo ndani ya pweza husaidia kupunguza athari za maradhi ya moyo kwa kuwepo mafuta ya omega-3 fatty acid.