Bikra inapimwa vipi na changamoto za kipimo hicho ni zipi?
Kipimo kinachoitwa kitaalamu kama two fingers virginity test ndio kinachotumika kuwapima wanawake hawa ubikra, mara nyingi madaktari hutumika kufanya vipimo hivi.vidole viwili huingizwa ndani ya uke kuangalia ile ngozi laini kwa jina la hymen ambayo inaaminika kutoka na kuchanika mwanamke anaposhiriki ngono kwa mara ya kwanza, wakikuta ile ngozi haipo basi mwanamke huyo sio bikra na wakikuta ngozi ile ipo basi mwanamke huyo ni bikra.
mpaka sasa hivi hakuna mashine maalumu au kifaa maalumu kinachoweza kusema kwa uhakika kwamba mtu huyu ni bikra. Lakini pia baadhi ya makabila huweka shuka nyeupe kwenye kitanda siku ya ndoa, damu ikimwagika basi huamini mtu huyo alikua bikra.
Sio rahisi kupima kama mwanaume ni bikra kwani wote wako sawa kimaumbile yaani mabikra na ambao sio mabikra.
Changamoto za kipimo hichi ni zipi?
Ngozi laini inayopimwa kutambua ubikra inaweza kuondolewa na baiskeli, kuendesha farasi au kufanya mazoezi mazito ya kukimbia na kuruka kamba, sasa mtu huyo anaweza kupoteza ngozi ile lakini kitaalamu yeye bado ni bikra kwani hajawahi kulala na mwanaume.
Wasichana wengine huzaliwa na ile ngozi ikiwa ndogo sana kiasi kwamba hata siku ya ngono kwa mara ya kwanza damu zinaweza zisitoke kabisa lakini mwanamke huyu bado ni bikra.
Baadhi ya wanawake ile ngozi inaweza kua ngumu sana na ikashindwa kutoka wakati wa ngono, kumbuka ngozi ile haizibiki kabisa tundu ndio maana damu za kila mwezi zinatoka hata kama mwanamke ni bikra.