Ukomo wa hedhi ni wakati gani?
Mwanamke huanza kupata ukomo wa hedhi (menapause) anapofika umri kati ya miaka 45-55. Wanawake wengine hupata ukomo wa hedhi angali na umri mdogo zaidi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kufanyiwa upasuaji au baadhi ya matibabu, kuugua au sababu nyingine.Katika hali ya kawaida, mwanamake huanza kupata hedhi chache anapofika umri wa miaka 40 ambapo huanza kupata mizunguko mirefu na inayobadilika mara kwa mara. Mizunguko huanza kuwa mirefu na baadaye kukoma kabisa.