Msichana huanza kupata hedhi (period) wakati gani?
Msichana huanza kupata hedhi (period) wakati gani?
Kwa kawaida, msichana huanza kupata hedhi ya kwanza (menarche) afikapo umri wa miaka 11-14. Hata hivyo, hedhi huweza pia kutokea binti angali na miaka 8 na hali hii huwa ni kawaida pia. Umri wa wastani ni miaka 12 lakini hii haimaanishi kwamba wasichana wote hupata hedhi ya kwanza katika umri sawa.Mara nyingi hedhi ya kwanza huanza miaka miwili baada matiti ya binti kuanza kutokeza. Iwapo binti hajapata hedhi ya kwanza angali na miaka 15 au ni miaka 2 hadi 3 baada ya kuanza kuota matiti, anapaswa amuone daktari.