Sifa na bei ya Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro 2019
Kwa kuanza labda tuanze kuangalia sifa za Tecno Camon 11 Pro, Simu hii mpya ya Camon 11 Pro inakuja na kioo cha inch 6.2 chenye ukingo wa juu maarufu kama notch, kioo hicho kimetengenezwa kwa teknolojia ya LCD pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixel na uwiano wa 19:9. Kwenye ukingo huo wa juu maarufu kama notch kuna kamera moja ya selfie yenye Megapixel 24 pamoja na sensor maalum kwaajili ya kusaidia sehemu ya AR emoji kufanya kazi vizuri. Sehemu hiyo ni kama ile ya kwenye iPhone X inayoitwa Animoji.Sifa za Tecno Camon 11 Pro
Ukubwa wa Kioo – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~269 ppi density).
Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) na HiOS 4.1
Uwezo wa Processor – Octa-Core 2.0GHz.
Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek Helio P22 Chipset.
Uwezo wa GPU – Mali-G71 MP2.
Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
Ukubwa wa RAM – GB 6.
Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye teknolojia ya AI pamoja na LED Flash
Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 16 na nyingine inakuja na Megapixel 5 zenye AI, Autofocus na Flash ya Dual-LED flash.
Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3750 mAh battery.
Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS. USB 2.0, USB On-The-Go.
Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black na Blue
Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM,), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Light Sensor, Compass, Proximity Sensor, Face ID Sensor na Fingerprint.
Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), na Ulinzi wa kutambua uso (Face ID).
Bei ya Tecno Camon 11 Pro
Kwa upande wa bei Tecno Camon 11 Pro inakuja ikiwa inauzwa kwa shilingi za Kenya Ksh 24,000 ambayo hii ni sawa na makadirio ya hadi Tsh 536,000 bila kodi. Kwa hapa Tanzania tegemea kupata simu hii kuanzia Tsh 550,000 au zaidi.