Saturday, January 19, 2019

Sifa 15 za kijana ambaye hajakomaa kwa ajili ya ndoa

Sifa 15 za kijana ambaye hajakomaa kwa ajili ya ndoa
1. Anaigiza maisha. 
Anataka kuonekana amefanikiwa kimaisha, hajui kuwa anajidanganya mwenyewe.

2. Hana mipango inayoeleweka, anajua kuzungumza lakini matendo ni sifuri, hajui kwamba kuanza mahusiano ni kubeba majukum.

3. Anataka ngono kabla ya ndoa, akipewa anasema binti hana hofu ya Mungu, asipopewa anatishia kuvunja mahusiano au anaanzisha mahusiano na msichana mwingine.

4. Ana wivu unaowaka kama moto wa nyika, anaweza kumkataza mchumba wake asiongee na mwanaume mwingine, au asifanye kazi kwa sababu boss wake anamtaka au kwa sababu anahisi kazi ile amepewa na 'mwanaume' .

5. Ana hasira mithili ya mbogo aliyechokozwa, anaweza kumpiga mpenzi wake au kumtukana. Ni katili, mdhalilishaji na anapenda kusikilizwa kwa kila amri atoayo.

6. Hajui lolote kuhusu Mungu, na hana muda wa kutafakari habari za Mungu.

7. Ni Tegemezi, anategemea wazazi au kupiga 'mizinga' kwa ndugu na marafiki ili kumudu mahitaji yake ya kila siku.

8. Si mtoaji kwa sababu hana kitu cha kutoa, ukimweleza shida yako hashindwi kukwambia we unapenda pesa, au anaweza kusema, 'Mi sio babako'

9. Anapowaza kuhusu ndoa anawaza ngono tu, hafikirii kuhusu majukumu ya kulea familia na mipango ya maendeleo ya familia.

10. Hajui kusifia, anachojua ni kukosoa tu. Anataka kupewa sifa zote hata ambazo hastahili.

11. Hujiona bora kuliko wengine na mara nyingi anapenda kushindana na watu bila sababu.

12. Anapenda maisha ya maonesho (show off) : 
Anaweza kupiga picha kwenye gari ya rafiki yake akaandika status, my new ride, anaweza kutamani hata kuombea mkopo; akipanda ndege basi hawezi kuwa na story nyingine zaidi ya safari ya angani. Akipata fursa ya kupiga picha na mtu maarufu basi anadhani na yeye ni maarufu na anadhani mafanikio ya mtu yule yamehamia kwake.

13. Mvivu, hawazi juu ya kesho yake. 
Anaanza mradi na kuishia mwanzoni (sio njiani) kwa sababu lengo ni kuwanasa wanawake wapumbavu.

14. Anashinda online anachat, na anajua wazi hakuna biashara anayofanya mtandaoni. Mitandao ya kijamii imeteka maisha yake, haongezi tija wala maarifa ya msingi kwa maisha yake.

15. Anazijua sifa zote za wife material lakini hana sifa hata moja kuwa husband material.

#AMKA KIJANA JITAMBUE#