Saturday, January 19, 2019

Jinsi ya kujua kama mwanamke anakupenda kimapenzi kabla hajakwambia

Jinsi ya kujua kama mwanamke anakupenda kimapenzi kabla hajakwambia
1. Anafanya mambo kukulenga
Mwanamke anayekupenda lakini hawezi kukwa mbia huwa anafanya mambo kukupima kama na wewe unampenda. Mfano wa mambo hayo ni kujifanya anaumwa na kuangalia wewe kiasi gani unamjali na kiasi gani utahangaika kwa ajili yake.

2. Haoni aibu kugusa sehemu yako ya mwili.
Msichana anayependa haoni aibu kukushika mkono ama kukutomosa au hata kukumbatia. Kwa kufanya hivyo hujua kuwa kwa asilimia kubwa hisia za kushikana kwenu kutamrahisishia kazi ya kuwa na wewe na kutakufanya wewe kujiskia kumpenda pia.

3. Kupenda kucheka
Mwanamke anayetaka ujue anakupenda huwa hucheka unapoongea au kufanya kitu chochote hata kama hakichekeshi. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli. Hii ni kufanya ili umtambue.

4. Anakuwa na Wivu
Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unaongea nao au ukichati nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi.

5. Anakumbuka siku zako muhimu
Mwanamke anayetaka ujue kuwa anakupenda hukukumbuka siku zako muhimu kama vile siku yako ya kuzaliwa hatoweza kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa au ukifaulu mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza. Hii ni kutaka kuwa karibu na wewe na kukuonyesha kuwa anakupenda.

6. Anaangalia machoni
Mwanamke anayekupenda anapenda kukuangalia machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utaelewa ni kiais gani anakupenda kupitia vile ambavyo anakuangalia. Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda si wote wana ujasiri wa kuwatazama wapenzi wao.

7. Anapenda kukaa na wewe
Mwanamke anayekupenda anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe. Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo.

8. Yupo tayari kujitoa.
Kama mwanamke anakupenda yupo tayari kujitoa sadaka. Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye anaweza akafanya kwa mtu mwingine. Yaani yupo tayari yeye akose lakini wewe upate na kwa mwingine anaweza akamwamba hana alichoombwa lakini akakupa wewe kama pesa na vitu vingine. Utaona ni vipi huyo mwanamke alivyo kwako na kwa wengine.

9. Anachukulia matatizo yako kama ni yake.
Unapomueleza kuwa ana tatizo anajali tatizo lako kama vile ni lake na hujisikia vibaya sana na kuhuzunika na atafanya lolote ili aweze kukusaidia utoke katika hilo tatizo. Mwanamke kama huyu huwenda anakupenda lakini ameshindwa kukwambia.

10. Hayupo tayari kuvunja urafiki
Kama mwanamke anakupenda na hamna uhusiano wa kimapenzi mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakuambia anakupenda. Kwa kuwa anakupenda endapo ikatokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose.