Friday, January 25, 2019

Sababu 6 kwa nini "unakojoa" mapema - Wanaume (Pre mature ejaculation)

Sababu 6 kwa nini "unakojoa" mapema - Wanaume (Pre mature ejaculation)
Pre mature ejaculation ni nini?
Hii ni hali ambayo mwanaume anatoa mbegu mapema sana kipindi cha tendo la ndoa na mara nyingi huambatana na kushindwa kumridhisha mpenzi wake.

Tatizo hili limekua likiwapata wanaume wengi na kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada  ya hali hii kutokea.

Kimsingi  mwanaume anatakiwa achukue dakika nne mpaka nane kabla ya kutoa mbegu za kwanza lakini watafiti wanasema tatizo hili hugundukiwa mtu anapotoa mbegu ndani ya dakika moja au kabla ya dakika moja.

Tatizo hili huweza kutokea mara tu baada ya kubalehe,{primary pre mature ejaculation} mda mrefu baada ya kubalehe{secondary PE} au kutokana na aina ya mwanamke uliompata.{situational PE}

Sababu 5 kwa nini "unakojoa" mapema - Wanaume (Pre Pre mature ejaculation)

Tatizo hili halina sababu za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila wanasayansi wanaamini sababu zifuatazo zinaweza kua chanzo kikuu cha tatizo hilo.

1. Kupiga punyeto au kujichua; 
Mara nyingi watu wanaopiga punyeto hua wanafanya haraka kwa kujificha ili wasikutwe na mtu. tabiaile ya kulazimisha mbegu zitoke haraka huweza kuleta tatizo hili.

2. Kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa; 
Kukaa mda mrefu sana bila kushiriki tendo la ndoa husababisha mkusanyiko mkubwa wa mbegu za kiume ambazo zinaleta msisimko mkubwa na ukichelewa sana kushiriki tendo la ndoa zitatoka kwenye ndoto nyevu. kawaida mwanaume anatakiwa ashiriki tendo angalau mara nne kwa wiki.

3. Kuwa na wasiwasi wakati wa tendo la ndoa; 
Mtu akiwa na historia ya kupata  hali hii kabla, hua hajiamini na kua na wasiwasi kwamba litatokea tena na matokeo yake hulipata kweli.

4. Madhara ya dawa zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu; 
Baadhi ya dawa za usingizi, mawazo na zingine zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu huleta tatizo hili mfano amitriptyline.

5. Kurithi; 
Baadhi ya koo au familia fulani hurithi vimelea vya kua na ugonjwa huu kwa vizazi mbalimbali vya familia husika.

6. Kutofanya mazoezi
Inashangaza kuwaona watu wenye uzito mkubwa kupita kiasi au wazee au wagonjwa ndiyo wapo mazoezini asubuhi na jioni. Ila wanaume wengi hawana bidii ya kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.

Hali ya ulegelege hupunguza uwezo wa mwanaume kushiriki tendo la ndoa na ndiyo sababu mojawapo ya upungufu wa nguvu za kiume.