Uhusiano kati ya Ute wa mwanamke na kubeba mimba - Ute wa mimba
Katika mlango wa uzazi hubadilika kulingana na siku mwanamke yupo katika mfumo wake wa uzazi (reproductive system circle). Hii hufanyika ili kuweza kuruhusu mbegu za mwanaume ziweze kwenda kwa kasi na kulifikia yai la mwanamke hivyo kurahisisha mwanamke kupata mimba.Hivyo basi ni muhimu kujua hili kama mwanamke kwa ajili ya kujilinda dhidi ya mimba usiyoitarajia au siku maalum za kulenga ili upate mimba kama unatafuta mtoto.
UTE UKIWA MKAVU AU UNANATA;
aina ya ute kama huu hauruhusu mbegu za kiume kusafiri na kuingia katika kizazi cha mwanamke hivyo mimba haiwezi kutungwa hapa, Huu ute huwepo mwanamke akiwa hayupo katika kipindi cha joto au kipindi ambacho yai yake bado halijapevuka.
UTE UKIWA NA RANGI YA KRIMU (Cream)
hapo mwanamke anakaribia kuingia katika kipindi cha joto pia yai linakaribia kupevuka bado hawezi kupata mimba.
UTE UKIWA MAJIMAJI AU YENYE UNYEVU UNYEVU;
huu unaweza kusafirisha mbegu ya mwanaume hadi kizazi cha mwanamke na kama imebaki siku mbili au tatu yai kupevuka ukifanya tendo la ndoa hapa kuna uwezo utashika mimba kwa sababu yai likipevuka litakutana na mbegu ya mwanaume ndani ya kizazi kuna uwezo mimba itatungwa. Mwanamke hupata hisia za kufanya mapenzi lakini siyo sana
UTE UKIWA NA RANGI NYEUPE KAMA YAI BICHI;
ute ukiwa katika hali hii ndiyo mzuri kabisaa kwa kusafirisha mbegu za kiume, pia hapa mwanamke ameshafika katika kipindi cha joto hapa tendo la ndoa likifanyika mimba inapatikana kwa asilimia zote kama hakuna vizuizi kutoka Mungu muumba na vizuizi vingine vya afya vinavyozuia mimba kutunga.
Hapa hisia za mwanamke za kufanya tendo la ndoa huwa juu sana na hutamani kufanya mapenzi kila mara especially yai likikaribia kushuka na likishuka. Ni muhimu sana mwanamke aangalie ute (vaginal mucus) katika kuzifahamu siku zake za kuweza kushika mimba na kutoshika mimba kuliko kutumia calendar ya damu ya mwezi.
Siku za ute ni siku 30 kinyume na siku za damu ya mwezi na pia ni muhimu sana mwanamke kushika ule ute kila siku kwa mkono wake kuangalia rangi na utelezi na harufu. Ongeza uwezekano wa kupata mimba kwa kutumia virutubisho vya tiba mbadala pamoja na Neplily sanitary pads kila wakati.