Dalili za mimba changa (Mimba ya siku tatu)
Dalili za mimba changa (Mimba ya siku tatu)
Dalili nyingine ni kuvimba matiti na chuchu kuchomachoma. Baadhi ya wanawake wanaota mavuzi mengi na wengine wengi rangi ya chuchu inabadilika kuwa nyeusi.
Pia, karibu nusu ya wanawake wajawazito huumwa tumbo na wengine hutapika. Wanawake wengi husikia mkojo mara kwa mara na wengine hujisikia wachovu na kuona kizunguzungu, hasa katika miezi mitatu ya mwanzo.
Wakati mwingine wanawake hupenda au huchukia baadhi ya vyakula. Ili mwanamke awe na uhakika kama ni mjamzito au hapana, akapimwe mkojo kwenye kliniki au hospitalini, mara anapokuwa na wasiwasi.