App ya Azam TV. App ya kisasa kabisa ya AzamTV imeanza kupatikana rasmi katika Google Play Store na App Store ya Apple kuanzia Julai Mosi.
App hiyo iliyokuwa ipatikane tangu Juni mosi lakini ilishindikana, watu wataweza kutazama chaneli saba ambazo ni Azam ONE, Azam TWO, Sinema Zetu, ZBC 2, Azam Sports HD kwa Tanzania Pekee, na Real Madrid TV na NTV Uganda.