Fahamu dalili hizi 9 kuwa wewe ni mchepuko tu!
Wanaume wengi ni wataalam wa kuwa na uhusiano na wanawake wengi kwa wakati mmoja. Sasa kwa msichana unayesoma makala hii, hizi ni dalili 9 kuwa huenda wewe si ‘baby number one’ wake bali ni mchepuko tu.Mazungumzo mengi naye yanahusisha kufanya mapenzi tu.
Hawezi kukualika kwenye mkusanyiko wa familia yake.
Hapendi surprises – hapendi uende kwake bila kumwambia.
Ni mkali sana kwenye simu yake, hawezi kukuruhusu uishike.
Ni mgumu kukuonesha mahaba ukiwa naye hadharani.
Anahofia kupiga selfie na wewe.
Anapigiwa simu za ajabu ajabu.
Hakuiiti wewe kama girlfriend wake. Akiwa na marafiki au ndugu zake anakutambulisha kwa jina lako.
Haongelei kuhusu mipango yenu ya baadaye