Tuesday, April 23, 2019

Mambo gani unapaswa kumfanyia mpenzi wako kila wiki? soma hapa


Mambo gani unapaswa kumfanyia mpenzi wako kila wiki? soma hapa
1. Umanatakiwa kupeana miadi ya kwenda mahala tulivu kabisa, mkibadilisha na mawazo. Sio kila siku kuwa chumbani, unachotakiwa ni kubadilisha mazingira. Wakati unapokuwa mnaelekea labda sehemu ya kubadilishana mawazo, usipende kutembea eti, mume nyuma mke mbele, kwani unamwogopa nani? Waonyeshe wale wanaojua kuchukua vya watu kwamba mmejenga ukuta imara wa penzi lenu. Watashindwa kutupa ndoana za kukuteka wewe ama mpenzio, Shikaneni mikono tena mkionyeshana kiasi gani mnapendana.

2. Mfanyia kitu ambacho wote mnaweza kukifurahia kwa kikifanya kwa pamoja.

3. Kama ni mwanamke unaweza kumpikia chakula kizuri ambacho anapendelae kukila, hakikisha chakula hicho kuanzia mapishi hadi kukiandaa mezani ni kazi yako. Sio Umpikie halafu umwambie 'hausigeli' akamwandalie, haipendezi kabisa na hata jisikia kula chakula chako.

Siajabu hata siku hiyo ya wikiendi unaweza kumlisha chakula hadi akashiba, sio kazi kumlisha mpenzio, unajua mwanaume ukimnyenyekea hukisikia ni bora na huongeza mapenzi zaidi.Atakudhamini kuliko chochote, atapenda kukuona mara kwa mara.

Mimi binafsi na mlisha mepnzi wangu, kwani nampenda sana. Ninapomlisha chakula akishiba nae hunilisha kwa furaha. Ninapomtamkia nimeshiba basi hunitolea tabasamu nono lililoshiba midomoni mwake.

4. Mpe mpenzio zawadi ya kumshangaza, ambayo unahisi ataipenda na kuifurahia.

5.Fikiria kitu ambacho utamfanyia wiki nyingine, hasa mapenzi. Usifanye mapenzi kila siku na pia hakikisha unabuni njia nyingine mpya ambazo atazipenda na kuzifurahia.