Tuesday, February 19, 2019

Njia muhimu 6 za kurefusha nywele za kiafrika hasa wanawake.

Wanawake wa kiafrika hua wana nywele fupi na ngumu, yaani hii ni asili yao tofauti na wanawake wa rangi zingine duniani kama wachina, wazungu, wajapani, wafilipino na kadhalika.. nywele za waafrika mara nyingi haziwi ndefu lakini kutokana na kubadilika kwa teknolojia, sasa hivi kuna uwezekano wa kukuza nywele zao kwa kufuata kanuni kadhaa za urembo na afya kama ifuatavyo.
Njia muhimu 6 za kurefusha nywele za kiafrika hasa wanawake.

1. Ziache nywele zako katika hali ya unyevunyevu
Kwa sababu ya ugumu wa nywele za kiafrika mafuta asili ya mwili yanachelewa sana kusafiri kutoka kwenye kichwa hadi mwisho wa nywele na kufanya zishindwe kukua kirahisi hivyo inatakiwa utumie mda mwingi kuzilainisha kwa kutumia conditioner rinse kila ukiosha nywele zako na kuiacha kwa dakika tatu mpaka tano kabla ya kuosha nywele kabisa na maji.
                                                             
2. Zipake nywele mafuta
Kwa sababu mafuta halisi yanayotengenezwa na mwili hayafiki kirahisi kwenye urefu wa nywele nzima basi ni vizuri kutumia mafuta mazuri ya nywele ili ziwe na afya tele na kuweza kukua.mafuta ya castrol oil au aloe vera yamekua yakitumika kwa miaka mingi kulainisha na kurefusha nywele.
                                                                 
3. Kata nywele zako pale inapohitajika
Nywele za juu au tip hua wakati mwingine zinakua kavu na nyekundu kutokana na kukosa mafuta hivyo kupunguza kasi ya nywele kukua hivyo ni vema kukata nywele hizo na kufanya zilizobaki ziongezeke urefu zaidi.

4. Meza virutubisho vya nywele
Virutubisho vya biotin mwilini hufanya kazi ya kukuza nywele, kuzifanya imara na kukuza kucha pia hivyo ukitumia vidonge hivi kama virutubisho husaidia nywele kukua. lakini pia vitaminin b6 husaidia ukuaji wa nywele kwa kuzuia kiwango cha hormone za uzazi yaani testestorene ambazo huzuia sana ukuaji na kufanya nywele ziwe nyembamba.

5. Zibane nywele zako; 
Sehemu ya juu kabisa ya nwele kama nilivyosema hapo mwanzo ni laini sana na hukatika kirahisi hivyo japokua kuana staili za wanawake kuachia nywele, zako kama bado ni fupi ni vizuri ukazifunga na kibanio ili zisikatike kirahisi.

6. Zifunike nywele zako na kilemba
Japokua sio rahiso kufunika muda wote ni vizuri ukazifunika wakati mwingine ila mafuta uliyopaka kichwani yasikaushwe na jua na pia wakati wa kulala ni vizuri kuzifunika ni nguo au mfuko wa jamii ya nylon ili mafuta uliyopaka yasiishie kwenye mto.

7. Tumia virutubisho vya protini; 
Protini ndio msingi wa binadamu yaani nywele, kucha, mifupa na na nyama zimejengwa kwa protini hivyo ni vizuri kutumia sana virutubisho hivi ambavyo mara nyingi hua vimetengenezwa kwa mimiea na wanyama na hufanya kazi zaidi kuliko hata protini tunazopata kwenye chakula lakini pia chakula cha protini kama nyama, samaki, karanga, korosho na dagaa ni muhimu sana kwa hili ndio maana watoto wenye utapiamlo hukonda sana na kua na nywele nyekundu zisizo na afya.