Tuesday, January 29, 2019

Mjue kuku mweusi tii wa ajabu anaepatikana nchini Indonesia

Mjue kuku mweusi tii wa ajabu anaepatikana nchini Indonesia
Ayam Cemani ni aina ya kuku mweusi anayepatikana nchini Indonesia. Kuku huyu ni mweusi titi kwanzia kichwani hadi miguuni na hata viungo vyake vyote vya ndani pia ni vyeusi.

Kuku huyo anaaminika kuwa wa kipekee na kiajabu pia. Kuku huyo hufugwa katika maeneo ya kisiwa cha Java.

Kwa mujibu wa imani za hapo toka karne ya 15 kipindi cha utawala wa mfalme Majapahit. kuku huyo aliaminika kuongeza baraka na nguvu katika eneo fulani na pia kuondoa bahati mbaya na balaa katika eneo anapofugiwa.
Katika maeneo ya sherehw na matamasha mbali mbali, kuku Ayam Jamani huchinnjwa ili kuondoa majanga na bahati mbaya. Wanasayansi wamefahamisha kuwa kuku huyo ni shifaa na ana manufaa mengi kwa mwili wa binadamu.

Kwa sababu hiyo nchini Indonesia kuku huyo huuzwa kwa kati ya dola 300 hadi 400 huku nje ya nchi kuuzwa kwa hata takriban dola elfu tano. Nyama na damu ya kuku huyo ni tiba kwa magonjwa hasa ya kifua kikuu na matatizo yote ya kifua.
Utafiti wa wanasayansi umedhihirisha kuwa rangi nyeusi ya kuku hiyo ni kwa ajili ya mabadiliko ya kizazi katika kanda ya bara la Asia. Mabadiliko hayo husababisha kuwepo na uzalishaji wa Melanini mwilini kwa mara kumi zaidi.