Karibu nusu ya wanawake hupata huzuni kali baada ya tendo la ndoa - Utafiti
Tendo la ndoa zuri linatarajiwa kukuacha ukiwa na furaha. Lakini karibu nusu ya wanawake hujikuta wakiwa na huzuni kali baada ya kufanya mapenzi, utafiti umesema.Hupata tatizo ambalo kitaalam linaitwa “post-sex blues” – linalotawaliwa na hali ya kutokwa machozi, huzuni kali, sonona (depression), kukerwa na hasira kwa takriban saa nne baada ya kufanya mapenzi.
Watafiti waliwauliza wanawake 230 wenye afya ya kushiriki tendo hilo kuanzia miaka 18 hadi 55 kuhusu ni mara ngapi hujisikia hali hii.
Walibaini kuwa asilimia 46 ya waliohojiwa walidai kuwahi kuwatokea walau mara moja katika maisha yao, huku asilimia 20 wakisema hupata hali hii mara kadhaa ndani ya wiki nne.
Hakukuwa na uhusiano kati ya ukaribu kati ya wapenzi na utokeaji wa post-sex blues, utafiti huo wa Australia uliochapishwa kwenye jarida la Sexual Medicine ulibaini.
Utafiti huo pia ulionesha kuwa baadhi ya wanawake hupata huzuni kubwa baada ya kufanya mapenzi kwakuwa wana historia ya unyanyasaji wa kimapenzi.