Wednesday, December 19, 2018

Wanawake wanavyojisikia kuhusu Tendo la ndoa, kabla na baada.

Wanawake wanavyojisikia kuhusu Tendo la ndoa, kabla na baada.
Wanawake wengi hupata hisia za kujamiiana wakiwa katika uhusianao mzuri na uliojaa upendo zaidi, na idadi kubwa ya wanawake wanaojihusisha na tendo hilo huchukulia kujamiiana kama tendo ambalo huleta muunganiko mkubwa wa kihisia katika mapenzi, mara nyingi uwezo wake wa utayari ndio humuwezesha kufika kileleni mara nyingi zaidi.

Zipo njia nyingi sana na tofauti ambazo wanawake huweza kutumia kuelezea hisia zao za tendo hilo kwa wenzi wao wa kiume.

Hizi ndio baadhi ya njia za kawaida ambazo wanawake wanaweza kuzitumia tofauti na wanaume.

Kujamiiana huanzia katika akili
Mara nyingi Wanaume hukata tamaa kwa kushindwa kutofautisha mabadiliko ya kihisia katika mwili wa mwezi wake wa kike, ni pale anapoona muitikio wa kihisia kimwili si sawa na wake vile anavyofanya. Lakini mwanaume anapaswa kukukumbuka kwamba miili yao imetofautiana kihomoni. Testosterone husababisha hamu ya kujamiiana kwa wapenzi wote kisaikolojia lakini kwa viwango tofauti, kwa kiasi kikubwa, jinsia ya kiume huwa na kiwango kikubwa cha homoni na hisia mara kwa mara kwa wakati huo wa kujamiiana. Kwa upande wa jinsia ya kike hisia hutokana na kukumbuka, na kufikiria tendo la kujamiana lililowahi kumvutia kwa kiasi kikubwa, ambapo huchochea kuongezeka kwa hali ya msisimko wa kujamiiana. Pia, mwanamke anapofikiria kuwa pamoja na mpenzi wake faragha mwanzoni mwa uhusiano hupelekea kusisimka zaidi na hamu yake ya kujamiiana huweza kuongezeka kwa urahisi.

Kujamiiana huanza na kutamani
Mtafiti wa masuala ya kujamiiana Meredith Chivers anasema “kutamani ni kufika kileleni”kwa wanawake. Kimtazamo (wanawake wengi wana mtazamo tofauti kuhusu wanaume wanaowavutia) mwanaume anayevutia anaweza kusababisha msisimko zaidi kwa mwanamke, hii ni kutokana na fikra zake binafsi,  wengi hujiuliza “je ananiona mwenye mvuto?”– jawabu la ‘ndio’ huleta athari chanya akilini mwake. Kujua kwamba mwenza wake ana hamu kwa ajili yake hali ambayo hupelekea kutamani kujamiiana kwa kiasi kikubwa. Kama vile wanaume mara nyingi wanatarajia tendo la ndoa mara nyingi baada ya kuoa, jambo ambalo hutarajiwa pia na wanawake wengi kupata mahaba yasiyokuwa na kikomo kutoka kwa wenzi wao kuendelea kushawishika kufurahia tendo la ndoa.

Kujamiiana ni mjumuisho wa vitu vingi
Wanawake wengi hupenda kujamiiana, lakini hamu ya tendo hilo huweza kuharibiwa kwa urahisi na uchovu, chuki, na matatizo ya kisaikolojia ya maumivu ya kumalizia. Wanawake hukosa wakati mwingi wa kufikiria kuhusu kujamiiana hii hutokana na kutokua mtu wa kumshawishi kwa ukaribu au historia yake ya dini na pengine kuwa na majukumu mengi ya kifamilia kama kuweka umakini kwa watoto, na kazi  za ndani. Mara nyingi wanawake huenda kitandani wakiwa na matarajio ya kufurahia tendo la ndoa na mahaba mazito licha ya miili yao kutokuwa tayari kufanya tendo hili la kujamiiana, hivyo wanawake huitaji maandalizi ya hali ya juu kwaajili ya kuamsha hisia zao. Na wakati mwingine kufikia kilele cha kuamsha hisia inahitaji maandalizi ya muda mrefu (kwa wanawake wengi inaweza kuchukua hata dakika 45). Si rahisi kufika kileleni mara kwa mara kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume. Hivyo, wakati wanaume wanapenda utofauti, wanawake wanaweza kupendelea nafasi iliyojaribiwa na ya kweli au mitindo mbalimbali ya kujamiiana iliowahi kufanyika na kutoa matokeo chanya ya kumfikisha kileleni kwa sababu kuna uwezekano zaidi wa furaha yake ambayo inamruhusu kupumzika kwa wakati.

Kujamiana kunategemea mazingira
Wakati wanawake wengi wanajifunza kujisisimua wao binafsi, pia kuna idadi kubwa ya wanawake inayoanza maisha yao ya kujamiiana wakiwa ndani ya uhusiano au ndoa. Lakini ukweli unabaki kuwa tendo la ndoa linahitaji ubunifu wa hali ya juu tena usiokuwa na kikomo hasa kama wapenzi wanataka kulifurahia tendo hilo daima kwa mfano; kubadilisha mazingira ya sehemu ya kujamiiana kama, kuweka rangi za kimahaba ambazo mwenzi wako anazipenda, kubadirisha mazingira kutoka sehemu iliozoeleka kama kutoka kitandani kwenda kwenye kochi au kiti, kutoka nyumbani kwenda hotelini na vitu vingine kama hivyo. Huweza kuongeza ushawishi na radha ya mapenzi.

Kujamiiana ni sehemu ya upendo
Kujamiiana, kuzungumza, kukumbatiana, kufanya kazi pamoja, kusimamia nyumba na familia kama timu, kusikia mapendekezo, kuadhimisha sikukuu, kutoa na kupokea zawadi, yote haya hujenga upendo kwa  mwanamke – kujamiiana ni sehemu ya yote hayo, sina haja ya kufafanua sababu. Kufanya mapenzi huweza kumfanya mwanamke alihisi joto la upendo, ingawa haimaanishi kuwa kujamiiana ndio chanzo kikuu cha upendo katika ndoa.

Kujamiiana ni njia ya mwanamke kuonesha upendo
Haina maana kwamba wanawake wanastahili kujamiiana wakati hawataki, lakini wakati mwingine anaweza kutambua haja ya mpenzi wake ya kufanya tendo na licha ya ukosefu wake wa hamu, anaweza kutaka kukidhi mahitaji ya mpenzi wake. Ikiwa kuna joto la uhusiano na mapenzi mema, kujitoa huku kunaweza kuwa zawadi halisi ya upendo. Ingawa ikisisitizwa inaweza kuvuruga juhudi zake binafsi kwa sababu jambo hilo linapaswa lifanyike na mwanamke kwa utayari wake.  Lakini jambo la kutia moyo ni kwamba wanawake wengi hujikuta wakifurahia tendo la ndoa baada ya kuanza hata kama hawakuwa tayari mwanzoni mwa tendo. Vilelile wanawake wengine huweza kuridhika kwa kujamiiana hata kama hajafikishwa kileleni. Mara nyingi tunataka kujisikia kama tupo sambamba na wapenzi wetu kabla ya kujamiiana, wakati mwingine ni kufanya tendo ambalo litatufanya tujiskie hivyo.