Yawezekana kweli ukawa na bahati mbaya ya kukutana na watu ambao si sahihi lakini leo acha nikupe mbinu sahihi za kumpata mwanaume sahihi.
1. Jitathimini mwenendo wako, ni rafiki kwa waoaji?
Kama kila siku wewe ni mtu wa viwanja, mtu wa kupenda starehe leo huku kesho huku jua kwamba kuolewa utachelewa sana.
2. Ishi kwenye mazingira ya kistaarabu.
Jiheshimu na sio kila siku kuwa mtu wa starehe, utaishia kuwapata watu wanaopenda starehe ambao mara nyingi nao huwa wana kasumba ya kubadilishabadilisha wanawake. Wanabadilisha kwa sababu maisha yao ni ya anasa. Kubadilisha wanawake pia kwao ni anasa, ni burudani na wanapenda kwelikweli.
3. Kwa imani fauta ile misingi ya dini, kama Muislamu nenda Msikitini na kama ni Mkristo nenda Kanisani.
Usiishi kama vile upo kwenye dunia yako. Usiwe na kasumba za chuki, kupenda ugomviugomvi kila mara na pia uwe mtu wa kujali matatizo ya mwenzi wako pamoja na roho nzuri kwa ndugu na jamaa wa mwenza wako.
4. Epuka kuwa na gubu.
Fungua moyo wako kwa mtu sahihi. Muombe Mungu akupe mume mwema, kubali kukosolewa, kubali kumsikiliza mchumba wako, atakupenda sana. Mheshimu mwanaume wako mtarajiwa, mpe heshima yake na yeye atakupenda sana! Kwa leo inatosha!
5. Kuwa na haiba ya kike.
Wanaume wengi waoaji huwa wanapenda kuoa wanawake wapole, wasikivu ambao hawapendi malumbano. Sio mwanamke unapenda malumbano kama kitu gani, wanaume hawapendi kelele nyingi kwani kiasili wanachoshwa na mihangaiko ya kila siku.
6. Wanaume wanapenda wanawake ambao wanaongea kidogo na kusikiliza zaidi.
Mwanamke ukiwa muongeaji sana, unaweza kuwakosa wanaume ambao hawapendi kelele. Jiweke karibu na Mungu, ishi katika misingi ambayo inakuonesha hata kwa macho tu kwamba una hofu ya Mungu.
Thursday, December 12, 2019
Ukiwa na sifa hizi 4 lazima uolewe haraka zaidi
WANAWAKE