Sababu 5 kuu kwa nini wanawake huwakataa wanaume
1. Kushindwa kujimudu kiusafiKuna baadhi ya wanaume hawazingatii masharti madogodogo muhimu ambayo yanafaa kuzingatiwa wakati wowote ule unapotaka kuongea na mwanamke. Usafi kwa mwanamke ni kitu muhimu sana ambacho huangalia kwa mwanaume.
Kwa wanaume kuvalia nguo nzuri na kuchana nywele ndilo jambo muhimu kwao lakini kwa mwanamke kiwango chake huwa ni cha juu. Kuanzia harufu mbaya ya kinywa, viatu vichafu, mshipi usiowiana na nguo, nyusi zilizokaa vibaya ni baadhi tu ya mambo ambayo mwanamke anazingatia kwa mwanaume.
Hivyo kabla hujatoka kwenda kutongoza msichana yeyote yule ama kwenda deti hakikisha ya kuwa umejiangalia kwa kioo na kuzingatia kila kitu ambacho utashuku kitamkwaza mwanamke.
2. Kujishasha
Kuna tofauti kati ya kujiamini na kujishasha. Kujishasha ni ile tabia ya kujisifu kwa vitu unavyomiliki, mambo ambayo umeyatimiza maishani mwako na tabia ya kujionyesha kwa watu. Mwanaume mwenye tabia hii bila kujua atakuwa akijisifu ili kumfurahisha mwanamke lakini kusema kweli ni kuwa tabia hii huwachukiza wanawake.
Pia kuwa mwanaume ambaye hamakiniki na mazungumzo ambayo anafanya na mwanamke, ama kumkatiza kati kati ya maneno mwanamke ili aongee yeye ni ishara ambayo itamboa mwanamke. Mwanaume mwenye confidence hawezi kusumbuliwa na vitu kama hivi manake anajiamini.
3. Kumkashifu mpenzi wako wa zamani
Kila mtu katika maisha yake ashawahi kuwa katika mahusiano ambayo hayakuenda vile yalivyotarajiwa. So kama ulikuwa na mahusiano mabaya mbeleni jiwekee wewe mwenyewe hayo mahusiano na hakuna mtu anataka kuyajua.
Tabia ya kuongea kuhusu mahusiano yako na mpenzi wako wa zamani na msichana unayemfukuzia ama kutongoza kutakufanya wewe uachwe. Hii inajitokeza pale mwanamke ataanza kuona ya kuwa wewe una maamuzi mabaya ya kuchagua wanawake. Pia anaweza kujiweka katika hali ya ex wako, ataona ya kuwa labda inaweza kufika pahala fulani pia yeye ukaanza kumkashifu kwa wanawake wengine.
Kama wataka kufanikiwa hapa usiwahi kumvuta mwanamke yeyote unayemtongoza kumuingiza kwa shida zako.
3. Kutokuwa na maamuzi
Cha kusikitisha mpaka karne ya leo kuna wanaume ambao hawawezi kufanya maamuzi wao wenyewe. Kila wakati anapotaka kufanya kitu lazima amuuliza mwenzake. Hii ni tabia ya mwanaume asiyefahamu lengo lake hapa duniani.
Iwapo kuna mwanaume ambaye kila wakati anamuuliza mpenzi wake kuhusu kila kitu anachotaka kufanya aidha kuanzia kumuuliza sehemu za kutembea wikendi ama chochote kile, basi mapenzi yao si marefu kwani itafikia mahali ambapo mwanamke atachukizwa. Hii ni moja ya sababu kuu ambayo inachangia wanaume wengi kuachwa kwa giza bila kuelewa tatizo la kuachwa lilikuwa lipi.
5. Uhitaji mwingi
Hili ni tatizo linaloongoza kuwa sababu kuu ya wanaume kukataliwa na wanawake. Uhitaji huu unaanzia kwa kutaka kuwa na mwanamke kila wakati, kubadilisha maisha yako ili yaambatane na yake, wivu mwingi ukitaka kujua wapi amekuwa siku nzima, kila wakati unampigia simu na kutaka kuhakikisha kutoka kwa marafiki zake, kukubaliana na kila kitu anachosema, kumwachia yeye atatue matatizo yenu, kumuomba ruhusa kwa jambo lolote unalotaka kufanya ni baadhi ya 'uhitaji' mwingi ambao wanawake huchoshwa haraka kutoka kwa mwanaume.