Sifa 9 nyingine za mwanamke zinzoangaliwa na wanaume tofauti na urembo
Mambo ambayo wanaume hupenda kwa mwanamke huwa mara nyingi hayana uhusiano wowote na jinsi mwanamke anavyoonekana kwa usoni au mwili wake ulivyo, japokuwa ni kweli muonekano wa sura au maumbile ya mwanamke ndio cha kwanza wanachokiona, na kushawishika mengine yafuate, humchukua mwanaume zaidi ya hayo mawili ili kufikia katika kufanya maamuzi ya kutaka kuishi na mwanamke mmoja wapo kati ya aliowahi kuwaona au kuwa nao kimapenzi, na muonekano na maumbile ya mwanamke huwa ni kitu cha mwisho kabisa kufikiriwa na mwanaume.Tumkuwekea hapa sifa za ziada ambazo mwanaume huangalia inapofikia hatua ya kutaka kuishi na Mwanamke au kumuoa kabisa.
1. Msikivu / Anayesikiliza.
Wanaume wengi hupenda sana kusikilizwa. Sauti yake iwe ni yenye kutoa amri ya mwisho katika familia. Hivyo mwanamke msikivu huwa na nafasi zaidi ya yule mbishi, mwenye kufikiria ushindani katika kila jambo maishani au kuhusi kamwe hawezi kuwa na mwanaume wa kumuamrisha.
2. Aliyeridhika au kujitosheleza
Wanawake wanaofurahia au kuridhika na wanachokifanya ni bora zaidi ya wenye kulalamika au kulalamikia hali fulani ya maisha anayoishi wakati uwezo wa kuyabadili upo mikononi mwake, kumbuka kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.
Haijalishi una uzuri kiasi gani, una kazi nzuri kiasi gani, au una CV yenye ukubwa upi, swala hili linagusia wewe kuwa na furaha na jinsi ulivyo kama mwanadamu(ridhika na ulivyoumbwa), kuwa na hali ya kuridhika na kile ulichonacho au ulichopewa na Mwenyezi Mungu.
3. Mpishi mzuri
Mabibi zetu walikuwa walishasema njia ya pekee kuukonga moyo wa mwanaume ni kwa kupitia tumbo lake, kila mtu anakumbuka hili na wala halina mjadala maana tumekua tukiyaona yanayotendeka kwenye familia nyingi sana. Siku hizi Wanawake kila kitu anaachiwa dada wa kazi. Kama unaishi na mchumba kwa sasa na unamfanyia hivyo, anakuchora tu….
4. Kuwa wa kweli ‘Don’t be too plastic’
Japokuwa wasichana ambao wamejitengeneza wanageuza sana shingo za watu mabarabarani, na kupata vinywaji vya bure kwenye sehemu za starehe, usiwaze!! Wanaume wengi kama sio wote, wanakubaliana kwamba kamwe hawawezi kumchagua mwanamke kama huyo kwa ajili ya kuwa na mahusiano zaidi mapenzi ya kawaida ‘a fling’. Kucha bandia, nywele za bandia, kope za bandia, kila kukicha amejipodoa, hiyo ni gharama ambayo hamna mwanaume anataka kuibeba maishani mwake.
5. Utayari wa kufikia muafaka ‘Easy to compromise with’
Kila mwanaume anajisikia vizuri akiwa anajua kwamba mwanamke wake yuko tayari kufanya makubaliano katika masuala yanayoihusu familia kiujumla na vile vile mwenye jitihada za kutafuta suluhu popote ambazo zitakubalika na pande zote mbili.
6. Mcheshi
Kama ana mpango wa kuishi na wewe basi angalau atahakikisha umcheshi kidogo, maana kununiana ndani ya nyumba sio vizuri, gubu kwa mwanamke halifai. Na vile vile watu wengi huhusisha ucheshi na uwezo mkubwa wa akili. Kuwa na mama mwenye uwezo kiakili ni dhahiri mtakua na kizazi chenye akili vile vile.
7. Ujasiri
Ni moja ya vitu ambavyo wanaume wengi hupenda kwa mwanamke, hii humpa moyo kwamba hata katika hali ambayo yeye hatakuwepo, mwanamke wake atamsaidia katika maamuzi yoyote yatakayohitajika kufanyika.
8. Kutokua feki kila wakati.
Make up usoni sawa inapendwa, lakini sasa isiwe maisha yako mpaka unasahaulika unakuaga vipi ukiwa Natural. Unaweza ukafikiri na kujiuliza, kama hii ni uso wako tu unautengeneza uwe feki kipi kingine unachokitengeneza ambacho hakiko sawa kwako.
9. Mchakarikaji ikifikia katika ule muda muafaka.
Mwanamke asie muoga na mwenye kujiweza na kujituma ikifikia wakati wa kuridhishana ni nyoongeza ya kutosha kwa Mwanaume endapo wewe ndo amekuchagua kuishi nae. Don’t be scared to get down & dirty.