Friday, January 4, 2019

Historia fupi ya maisha ya Rose Muhando

Historia fupi ya maisha ya rose muhando
Rose Mhando ambaye hujulikana pia kwa jina la Rose Muhando; amezaliwa mwaka 1976 katika kijiji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania. Ni msanii maarufu wa muziki wa injili katika lugha ya swahili katika kanda ya Afrika Mashariki.

Rose Muhando, ambaye alikuwa muumini wa dini ya kiislamu, ni mama wa watoto watatu. Rose Muhando alidai kuwa akiwa na umri wa miaka tisa alipata maono ya Yesu Kristo akiwa amelazwa. Aliteseka kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya hapo alipona na kubadili dini (kuongoka) na kuwa mkristo.

Alianza fani yake ya muziki kama mwalimu wa kwaya inayoitwa Kwaya ya Mtakatifu Maria katika kanisa la kianglikana linaloitwa Chimuli mkoani Dodoma.

Mnamo tarehe 31 mwezi Januari mwaka 2005, Rose Muhando alipata tuzo ya mtunzi bora, muimbaji bora, na tuzo ya msanii mwenye albamu bora ya mwaka wakati wa tamasha la tuzo za kiinjili, 2004.

Mnamo mwezi wa kumi na mbili, 2005, alishiriki katika tamasha la kiinjili ili kusaidia kutafuta fedha kwa ajili ya kituo cha watoto yatima cha Dar es salaam.

Baadhi ya albamu zake ni pamoja na:

1. Kitimutimu.

2. Uwe Macho, 2004.

3. Jipange Sawasawa, 2008.

Source: Wikipidia