Wednesday, December 26, 2018

Madhara ya kutazama video za ngono

Madhara ya kutazama video za ngono
Video za ngono zinaathiri kubwa. Watafiti wanasema kwamba “kutazama video za ngono kunaweza kuwafanya watazamaji wafanye ngono potovu.” Ripoti hiyo inasema “imeonekana kwamba wanawake husababisha na hufurahia ubakaji, na kwamba ubakaji ni jambo la kawaida sana katikati ya wanaume ambao hutazama Video za ngono”

Watafiti fulani wanasema kwamba kutazama Video za ngono kunaweza kuathiri uwezo wa kufurahia na kufanya ngono katika ndoa. Dakt. Victor Cline, mtaalamu wa kutibu watu wanaotawaliwa na mambo ya ngono, ametambua kwamba watu wanaotazama Video za ngono huendelea tu bila kuacha.

Mtu anayeanza kutazama Video za ngono kidogo-kidogo, asipoacha mwishowe anaweza kuwa na zoea la kusoma habari na kutazama Video za ngono. Cline anadai kwamba zoea hilo linaweza kuongoza kwenye matendo mapotovu ya ngono.

Wanasayansi wanaochunguza tabia za wanadamu wanakubaliana na jambo hilo. Dakt. Cline anaripoti kwamba “upotovu wowote wa ngono unaweza kuanza hivyo . . . na kwamba mtu hawezi kuacha hata akisumbuliwa sana na dhamiri.” Hatimaye, huenda mtu anayetazama Video za ngono akajaribu kufanya mambo yasiyo ya adili aliyoona, na mara nyingi matokeo huwa mabaya.

Tatizo hilo linaweza kuanza hatua kwa hatua bila kutambuliwa, asema Cline. Aongeza: “Huongezeka na kuenea kama kansa. Kwa kawaida zoea hilo halikomi, wala haliwezi kutatuliwa kwa urahisi.

Haishangazi kwamba mara nyingi wanaume waliozoea kutazama ponografia hawakubali kwamba wana tatizo, na ni kawaida kwa wenzi wa ndoa kukosana, nyakati nyingine kutalikiana, na hata mahusiano mengine ya karibu huharibika kwa sababu hiyo.”